Duration 4:31

SHAMIM, MUMEWE WAKUTWA NA KESI YA KUJIBU MAHAKAMA YA MAFISADI MASHAHIDI WANANE

25 160 watched
0
113
Published 2 Sep 2020

Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imemkuta na kesi ya kujibu Mfanyabiashara Abdul Nsembo na Mkewe Shamim Mwasha wanaokabiliwa na mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya. Jaji Elieza Luvanda alisema upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi nane pamoja na vielelezo sita ili kuthibitisha mashitaka hayo. Alisema mahakama baada kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, umeona washitakiwa Nsembo na Shamimu kuwa na kesi ya kujibu. Jaji Luvanda alipanga Septemba 3, mwaka huu (kesho) kwa washitakiwa hao kuanza kujitetea ambapo walidai watakuwa na mashahidi watatu ikiwamo wao wenyewe. Upande wa mashitaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Veronica Matikila vielelezo vilivyoambatanishwa kwenye kesi hiyo ni maelezo ya onyo kwa washitakiwa wote wawili, hati ya ukamataji, ripoti ya uchunguzi wa maabara ya Serikali, fomu ya kuwasilisha sampuli maabara, taarifa ya usajili wa gari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na bahasha zilizokuwa na dawa za kulevya.

Category

Show more

Comments - 31