Duration 2:50

Tume ya Uchaguzi yapongezwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa 2020//Changamoto zilizojitokeza kumalizwa.

36 watched
0
0
Published 13 Jul 2021

#NEWS RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi kwa Watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na Wadau wote wa Uchaguzi kwa kufanikisha vyema Uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba 28, mwaka 2020. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kumkabidhi Rais Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa kumchagua Rais wa Zanzibar, kuwachagua Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Madiwani na kuvihusisha vyama 19 vya siasa. Katika pongezi hizo, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba kuna kila sababu ya kutoa pongezi kwa wadau wote wa Uchaguzi wakiwemo Tume husika, Vyombo vya Ulinzi na Usalama,Asasi za Kiraia pamoja na wananchi wote kwa Ujumla kutoka na kwenda vyema kwa zoezi la uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020. #SiteNews #TukutaneSite #TukutaneKazini

Category

Show more

Comments - 0