Duration 1:52

Mhe. Prof Kabudi aipongeza LSF kwa kuwezesha upatikanaji wa haki nchini

22 300 watched
0
36
Published 28 Oct 2021

Kauli ya Waziri wa Katiba na Sheria nchini, Profesa Palamagamba Kabudi mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kuhusu kazi inayofanywa Shirika la Legal ServicesFacility (LSF). "...Mheshimiwa Rais tunaandaa programu ya 'primary legal services' - huduma za sheria katika ngazi ya msingi, kama ambavyo tuna intergrated judicial system katika ngazi hii. Twende sasa katika ngazi za vijiji. Mahakama za mwanzo zile zifanye kazi pamoja na paralegals ambao wapo ndani ambao wanatambuliwa na Sheria ya Msaada wa Kisheria. Na kwa hili nimshukuru sana Lulu Ng’wanakilala wa Legal Services Facility. Anatusaidia sana katika paralegals. Huduma ya msingi ya sheria itategemea sana paralegals. Na Mheshimiwa Rais ili kuwafanya paralegals na wao wajisikie tunaanza mpango wa mafunzo wa ngazi ya cheti ili na wao wahitimu wawe na cheti ili mawakili wasidhani hawa ni watu ambao hawana elimu au hawana maarifa. Na pia tunaandaa ngazi ya diploma ili na wao wasome wahitimu. Hawa ndio watakuwa wahudumu wakubwa katika ngazi ya mahakama za mwanzo kwasababu mawakili wapo lakini mawakili wanataka kipato. Na kipato ambacho yawezekana kabisa watu wa chini hawawezi. Kwahiyo, Mheshimiwa Rais tutakuja na programu kubwa chini ya uongozi wako ya huduma za sheria kwa ngazi za msingi..." Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Tanzania Gender Bench Book On Women's Rights kilichoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).

Category

Show more

Comments - 6